Jumamosi, 28 Septemba 2013

HISTORIA YA KWELI SEHEMU YA WANZA (1).








"HISTORIA YA KWELI"

Email:Nicodemoe.nicodemo@rocketmail.com
                             Au     :Nicodemoemmanuely@gmail.com
Phone:+255767-110 042,+255779110042, +255658-110 043,+255684843810
 
         Naitwa Nicodemo Emmanuely Nicodemo, nimezaliwa tarehe 19 Novemba 1989 katika Mkoa wa Shinyanga, Mama yangu anaitwa Getruda Mathias na Baba yangu anaitwa Emmanuely Nicodemo. Mimi ni mtoto wa kwanza katika upande wa mama, vile vile ni mtoto wa kwanza katika upande wa baba. Ukweli ni kwamba baba na mama yangu hawakuweza kuishi pamoja sababu baba yangu alimdanganya mama yangu kuwa atakuja kumuoa lakini kumbe yalikuwa ni maneno ya mdomoni tu!, hivyo aliamua kwenda kuoa kwingine alimuacha mama yangu akiwa ni mjamzito ndani ya tumbo hili alikuwemo mototo wa kiume ambaye ndio mimi Nicodemo. Kiukweli kuanza nazaliwa mpaka nafikisha umri wa miaka mitano (5) nimelelewa na mama. Mama yangu alikuwa akiishi na dada yake katika Mkoa huu wa Shinyanga.

    Baada ya kukaa kwa miaka mingi Mkoani Shinyanga Dada yake mama pamoja na mume wake Dr.Malale waliamua kuhama na kuhania Mkoa mwingine ambao ni Mkoa wa Dar-es-salaam na kuanzisha makazi mengine, huko nilibaatia kuonana na ndugu wengine ambao nilikuwa siwafahamu. Nilimuona kaka yake mama ambaye mimi nilikuwa namuita Mjomba, jina lake alikuwa anaitwa Venance Mathias yeye alikuwa anafanya kazi katika Shirika ya umeme (Tanesco) yeye pia alichangia katika kumtunza mama yangu kwa sababu mama yangu alikuwa hana kazi ya aina yeyoye.  Iliniuma sana kuona mama yangu akiwa ananyanyasika lakini nilikuwa sina jinsi.

    Ilipofika mwaka 1998 nilipelekwa kuandikishwa shule darasa la kwanza katika shule ya msingi Mtoni, watoto wa baba yangu mkubwa Dr.Malale wenyewe walipelekwa shule ya msingi Kisutu wao walikuwa wamenitangulia darasa.

    Siku moja mama yangu Mkubwa dada yake mama katika mizunguko yake ya hapa na pale alibaatika kukutana na kaka yake baba ambaye alijulikana kwa jina la Abeli Nicodemo hivyo mama yangu mkubwa alimuomba afike nyumbani kwa ajili ya kutambuana zaidi kwani ni miaka mingi hawakuweza kuonanana. Ndipo alipofika nyumbani nakutukuta tukiwa tunacheza. Nipo mama mkubwa alipo mtambulisha na mwambia kuwa mimi ni motto wa mdogo wake Emmanuely ndipo na mimi ndipo nilipomfahamu kwa mara ya kwanza. Ikam-bidi na yeye kutuchukua na kutupeleka nyumbani kwake kwenda kupafahamu, hivyotuliondoka nyumbani tukiwa watatu mimi pamoja na watoto wawili wa baba yangu mkubwa Dr.Malale tulifika mpaka nyumbandi kwake yeye alikuwa anaishi Yombo Dovya na sisi kwa kipindi hicho tulikuwa tunaishi Tandika, kuanzia siku hiyo tulikuwa tunakwenda kumtembelea siku za jumamosi kwa sababu siku hiyo huwa hatuendi shule. Hadi ikafikia kipindi mimi kulazimika kuamia kwake na kuishi huko ndipo nikawa naonana na baba yangu huko kwani alikuwa akitoka Shinyanga kuja Dar-es-salaam alikuwa akifikia kwa kaka yake huyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

AMTOROKA MME WAKE NA KUKIMBILIA KUSIKOJULIKANA

AMTOROKA MME WAKE NA KUKIMBILIA KUSIKOJULIKANA                  ...