ILE Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya
GPL imeshuhudia mume wa mtu aliyejitambulisha kwa jina la Emmanuel
Benedict na mke wa mtu aitwaye Rehema ambao wamenaswa laivu wakifanya
‘mambo’ gesti.
Wawili hao walinaswa hivi karibuni
kwenye gesti ambayo pia ina baa iitwayo Blue Roze maeneo ya
Buguruni-Sokoni jijini Dar wakijiachia kwa raha zao.
Habari zilizopenyezwa katika timu
yetu ni kwamba, baa hiyo hutumia vibaya leseni yake ya biashara kwa
kugeuza gesti hiyo danguro ambapo machangu hufanya biashara ya kuuza
miili yao katika eneo hilo.
Ilielezwa kuwa baa hiyo huwahifadhi
machangudoa ndani yake huku biashara ya ngono ikifanyika mchana kweupe
na usiku kucha bila kushtukiwa.
KAZI YAANZA
Ikiwa imebeba kauli ya Kamishina wa
Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Suleiman Kova kuhusiana na
kukomesha biashara ya madanguro jijini, vijana wa OFM walitinga ndani ya
baa hiyo kama wateja na kukamilisha uchunguzi wao ambao uliwapa jibu
moja tu – biashara ya ngono inafanyika nje nje!
Wakati huohuo, kijana mwingine wa OFM
aliingia upande wa gesti iliyopo ndani ya baa hiyo ili kupeleleza bei
zake huku mhudumu akiahidi kupunguza bei kwa kuwa alikuwa na changudoa
kutoka ndani ya baa hiyo tofauti na wengine waliokuwa wanatoka nje ya
eneo hilo.
TAARIFA POLISI
Baada ya kujiridhisha kuwepo kwa hali
hiyo, OFM ilitoa taarifa kwa Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Ilala, Lucy
Kakulu ambaye haraka alimtaarifu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala,
Marietha Minangi ambaye muda mfupi baadaye aliwasili kituoni hapo na
kutoa baraka kwa OFM na kushiriki kuwachagua askari shupavu wa kufanya
oparesheni hiyo
Ilipotimia usiku wa manane, ndipo
zoezi zima lilianza kwa mmoja wa mapaparazi wetu kuingia ndani ya baa
hiyo na kupitiliza moja kwa moja hadi ndani ya gesti.
Akiwa ndani, paparazi huyo
alifanikiwa kupatana na mmoja na kuingia naye chumbani huku akitoa
ishara kuwa kila kitu kilikuwa wazi ni kiasi cha zoezi kufanyika tu.
KAZI IKAANZA
Kufumba na kufumbua askari shupavu wa
Kituo cha Polisi Buguruni, Dar sambamba na timu ya OFM waliingia
mzigoni ambapo waliwanasa machangudoa na meneja wao aliyekuwa akizagaa
ndani ya gesti hiyo.
Katika pekuapekua hiyo ndipo mume
huyo wa mtu akanaswa laivu chumbani na mke wa mtu huku wote wakiomba
msamaha kwa kuwa wana familia zao, hoja ambayo haikuwa na nguvu.
KILA MTU ANA NDOA YAKE
Katika kurusharusha miguu, mwanaume
huyo alisema anaomba sana ishu hiyo iishie hapo, isifike polisi wala
kwenye vyombo vya habari kwani ana ndoa na familia hivyo itakuwa ni aibu
kubwa.
“Chondechonde mimi nina ndoa na
familia jamani. Sijui nitaweka wapi sura kwa aibu. Naombeni tuyamalize
kiutu uzima,” alisikika mwanaume huyo akijitetea kwa polisi, utetezi
ambao haukumsaidia.
Katika mahojiano huku kondom
zilizotumika zikiwa zimezagaa kila kona, kwa upande wa mwanamke alikiri
kuwa alifanya tendo hilo bila kinga.
“Hatujazitumia sisi hizi, tumezikuta
humuhumu chumbani. Lakini nawaombeni sana, msinipeleke polisi nina ndoa
yangu. Naombeni mnisamehe kwa sababu mume wangu atanirarua. Ninyi
wenyewe mnajua ndoa ilivyo ngumu, tafadhali naomba mnisitiri,” alisikika
mwanamke huyo.
SAFARI YA POLISI
Pamoja na kuomba sana, polisi hao
waliokuwa makini na kazi yao wakionekana kumuunga mkono vilivyo Kamanda
Kova, waliwatilia ngumu na kuamua kuondoka nao wakiwa na pingu mikononi
mwao.
Mbali na hao, oparesheni hiyo pia
ilimtia nguvuni meneja wa eneo hilo, Emmanuel Mpinge, ambao wote kwa
pamoja walifikishwa kituoni na kufunguliwa kesi yenye namba
BUG/RB/13114/2013 - KUFANYA VITENDO VYA UMALAYA 19/10/2013.
"COMEDY PRODUCTIONS ,PHOTOS EDITIONS, WELDING EVENTS,NEWS AND OTHERS UNDER NICODEMO STUDIO"
Jumamosi, 26 Oktoba 2013
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
AMTOROKA MME WAKE NA KUKIMBILIA KUSIKOJULIKANA
AMTOROKA MME WAKE NA KUKIMBILIA KUSIKOJULIKANA ...
-
Africa ni Bala linalopendwa na watu wengi Duniani na ina vivutio vya aina ya pekee kulio maeneomengine duniani kote hivyo twajivunia ...
-
ILE Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya GPL imeshuhudia mume wa mtu aliyejitambulisha kwa jina la Emmanuel Benedict na mke wa mtu aitwaye R...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni