Stori: Shakoor Jongo na Musa Mateja
MKALI wa songi linalotamba runingani
na redioni ndani na nje ya Bongo la Number One, Nasibu Abdul Juma
‘Diamond Platnumz’ amefunguka na kuanika siri tano za kurudiana na Wema
Isaac Sepetu ‘Madam’.
Wiki mbili zilizopita, wakiwa Hong
Kong, China, vyombo vya habari na mitandao ya kijamii viliripoti
kurudiana kwa Diamond na Wema waliomwagana takriban mwaka mmoja uliopita
ambapo staa huyo wa Bongo Fleva aliibuka na kukanusha vikali akidai
kuwa picha zinazomwonesha yuko na Wema ni za Filamu ya Temptations.
Akizungumza na Risasi Jumamosi kwa
dakika ishirini katika mahojiano maalum jijini Dar mara tu baada ya
kutua kutoka China Jumatano iliyopita, Diamond alikiri kufaidi penzi la
Miss Tanzania huyo wa mwaka 2006.
Diamond alisema kuwa, Wema ndiye
aliyetangulia kwenda China ambapo yeye aliungana naye siku kadhaa
baadaye akitokea kwenye shoo nchini Malaysia.
SIRI YA KWANZA
Akianika siri za kujikuta mikononi
mwa mwigizaji huyo mwenye mashabiki wengi zaidi katika tasnia ya filamu
za Kibongo, Diamond alisema kwanza ni ukarimu aliopewa na mrembo huyo.
Alisema kuwa alipotua Hong Kong alishangaa kukutana na mapokezi ya Wema kwenye uwanja wa ndege jambo ambalo hakulitegemea.
“Alinionesha ukarimu wa hali ya juu mno. Wakati tulipokuwa hapa Bongo tulikuwa hatusalimiani.
“Kuna vitu vingi vya ajabu vilitokea
huko nyuma kati yangu na Wema. Sikufikiria wala kuwaza kama anaweza
akawa mkarimu kwangu kiasi kile.
Akaongeza: “Kwa mazingira
yalivyokuwa, kwa namna yoyote lazima mwanaume aliyekamilika arudishe
moyo nyuma na kuacha mambo mengine yaendelee.
“Kiukweli nisema tu kuwa hata tungekutana Morogoro au Dodoma kwa ukarimu ule mwisho wa siku tungerudisha uhusiano wetu.”
SIRI YA PILI
Diamond alisema baada ya mapokezi ya
nguvu, Wema alimpeleka kwenye hoteli ya nyota tano (five stars) ambapo
huko alipatiwa huduma ‘klasiki’ na kujiona kama yupo kwa mama Nasibu
vile.
SIRI YA TATU
Alifunguka kuwa kitendo cha Wema kuwa
mwenyeji wake China ambako alikuwa mgeni hadi akapazoea nacho ni siri
nyingine iliyochangia wao ‘kukumbushiana’.
SIRI YA NNE
Alisema kuwa mwanadada huyo
alimuonesha mapenzi mazito (yaani kutekwa kimapenzi) hivyo haikuwa
rahisi kumchomolea kwani waliishi kama ndiyo penzi jipya linachipuka,
akajikuta akiogelea naye.
SIRI YA TANO
Diamond alisema kuwa bado ana ndoto
ya kupata mtoto kupitia kwa Wema ambaye anajua kuwa alishamwambia lengo
lake juu ya kupata naye uzao hivyo katika nyakati za kukutana kwao
anaamini ndoto itatimia.
HAKUNA CHA FILAMU
Alipoulizwa juu ya madai kuwa
walikuwa wakirekodi filamu, Diamond alifunguka kuwa hakuna cha filamu
wala sinema na kama kuna mtu anasubiri filamu atakaa sana.
“Naomba nikiri kuwa kweli zile picha
hazikuwa za filamu wala nini bali ndivyo hali halisi ilivyokuwa kati
yangu na Wema kule China.
“Pia naomba niseme kuwa uhusiano wetu
wa kimapenzi uliishia China na sasa hivi tumebaki kama kaka na dada na
ni ruksa kila mtu kumtumia mwenzie katika kazi mbalimbali kama ataona
kuna ulazima wa kufanyika hivyo,” alisema Diamond.
Hii ni mara ya kwanza kwa Diamond au
Sukari ya Warembo kukiri kuwa kweli alirudisha penzi lake kwa Wema
walipokuwa nchini humo wakijiachia.
PENNY HANA CHAKE?
Kwa mujibu wa watu wa karibu wa
Diamond, ukifuatisha simulizi hiyo ya mapenzi kati ya msanii huyo na
Wema, ni dhahiri kuwa mpenzi wa sasa wa jamaa huyo, Penniel Mungilwa ‘VJ
Penny’ hana chake kufuatia usaliti huo.
Hata hivyo, jitihada za kumtafuta
Penny ziligonga mwamba kufuatia simu yake kuita bila kupokelewa lakini
juzi wanahabari wetu walipofika nyumbani kwa Diamond, Sinza-Mori, Dar
waliambiwa mrembo huyo alilala hapo na kuondoka asubuhi.
GPL
"COMEDY PRODUCTIONS ,PHOTOS EDITIONS, WELDING EVENTS,NEWS AND OTHERS UNDER NICODEMO STUDIO"
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
AMTOROKA MME WAKE NA KUKIMBILIA KUSIKOJULIKANA
AMTOROKA MME WAKE NA KUKIMBILIA KUSIKOJULIKANA ...
-
Africa ni Bala linalopendwa na watu wengi Duniani na ina vivutio vya aina ya pekee kulio maeneomengine duniani kote hivyo twajivunia ...
-
ILE Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya GPL imeshuhudia mume wa mtu aliyejitambulisha kwa jina la Emmanuel Benedict na mke wa mtu aitwaye R...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni