Habari Wadau:
Dini inayoamini katika MUNGU lakini
ikiruhusu yale ambayo dini zingine zinapinga imeanzishwa eneo la mji
mdogo wa Makongolosi wilayani Chunya mkoani Mbeya,
Dini hiyo haiamini katika kutoa
sadaka bali inasema tunamtolea nani sadaka wakati Vitu vyote
tulivyonavyo ni mali ya MUNGU,kwa nini tunampa MUNGU mali zake Mwnyewe.!
Dini hiyo inaruhusu ulevi,uchawi na
uzinzi kwa sababu vimeumbwa na MUNGU,Vile vile inaamini hakuna dhambi
duniani,Dini hiyo inaitwa DIMAYO, sasa imeanza kuenezwa Mbeya
=========================
Ufafanuzi
=========================
Quote By GAMBISHI DWESE View Post
Yawezekana kweli Bwana Domy umekutana
nami. Mimi Ndiyo PAPA-DIMAYO 1: GAMBISHI DWESE,( nabii wa kwanza wa
DIMAYO) hata hivyo pengine umeninukuu kimakosa.Kwanza kabisa Dimayo
haiamini katika uwepo wa mungu muumbaji aliye hai wala aliyekufa
anayedaiwa kuhusika na kila kinachoendelea ulimwenguni.
Na nimeshatoa kitabu kinachoitwa
HAKIKA HAKUNA MUNGU MUUMBAJI ALIYE HAI WALA ALIYEKUFA anayehusika na
kila kinachoendelea. kijitabu hiki kinaeleza kinagaubaga kwanini Dimayo
haiamini katika uwepo wa mungu muuumbaji. nikipata nafasi nitakiingiza
kwenye mtandao ili watu wengi wakisome.
Ni kweli hakuna kitu Dhambi bali kuna
makosa. na kosa linaweza kuwa kosa kulingana na mazingira na wakati
katika jamii tofauti. Na ni kweli kwamba dini yetu ni ya starehe wala si
ya mateso, maana tunaamini hakuna maisha zaidi ya haya tuliyonayo.
Dimayo haijampa mtu ruksa ya kuvunja kanuni halisi asili wala sheria
halali ya serikali yake halali na wala haina upotoshaji hata kidogo.
Kinachoitwa sadaka kwetu huwapa watu
wenye matatizo. Ni kweli kuna michango mingine lakini ni ya hiari na ni
kwa ajili ya ushirika. Ni kweli kwenye JUMADI (jumba la makutano la
Dimayo kutakuwa na kaunta ya vinywaji). unajua kunywa na ulevi ni vitu
viwili tofauti; ulevi ni tabia ya mtu ya kutumia vileo kupindukia,
lakini kwetu tunasema kunywa uwezavyo ilimradi huumii wala kuumiza vyote
kisaikolojia na kimwili, kwa mantiki hiyo ulevi kwetu noma ila unywaji
ni safi.
Uchawi ni sayansi, ila utumike kwa
faida siyo kwa kuleta madhara. kuwaambia watu eti acheni ngono eti mungu
hapendi wataacha?. wambie wafanyeje ngono kulingana na wakati na
mazingira. Dimayo inamfundisha mtu kutenda inavyofaa yanayofaa kutendwa
kwa kufuata kha na kahaka. Anyway nashukuru kwa kuianzisha mada hii,
nafikiri nitachukua nafasi kuielezea zaidi kila inavyowezekana. Nina
uhakika kwa mtu yeyote mwenye uwezo mkubwa wa kutumia akili zake hawezi
kupingana hata kidogo na DIMAYO.
"COMEDY PRODUCTIONS ,PHOTOS EDITIONS, WELDING EVENTS,NEWS AND OTHERS UNDER NICODEMO STUDIO"
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
AMTOROKA MME WAKE NA KUKIMBILIA KUSIKOJULIKANA
AMTOROKA MME WAKE NA KUKIMBILIA KUSIKOJULIKANA ...
-
Africa ni Bala linalopendwa na watu wengi Duniani na ina vivutio vya aina ya pekee kulio maeneomengine duniani kote hivyo twajivunia ...
-
ILE Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya GPL imeshuhudia mume wa mtu aliyejitambulisha kwa jina la Emmanuel Benedict na mke wa mtu aitwaye R...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni