Jumatatu, 27 Januari 2014

AJALI MBAYA YA GARI AINA YA NOAH NA LORI MKOANI SINGIDA,WATU 13 WAFARIKI PAPO HAPO LEO

Gari ya abiria aina ya Noah imepata ajali mbaya baada ya kugongana uso kwa uso na Lori,hali iliyopelekea gari hilo la abiria (Noah kuburuzwa na kutupwa kando kando ya barabara kama lionekanavyo pichani mapema leo asubuhi,ajali hiyo imetokea kijiji cha Issuna,kijiji cha kwanza kutokea Manyoni mkoani Singida likielekea Mkoani Dodoma.
Ajali hiyo ya kusikitisha ilitokea huku mvua kubwa ikinyesha eneo hilo,hali iliyopelekea kupata msaada haraka kuwa ya taabu,Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani Singida alibainisha kuwa marehemu wote na majeruhi walikimbizwa hospitali Mkoani Singida.
Aidha mpaka sasa imekuwa vigumu kujua idadi kamili ya abiria waliokuwa kwenye gari hiyo aina ya Noah,hali inayopelekea pia utata wa kutambua majina ya marehemu.Katika ajali hiyo Dereva wa Lori na Kondakta wake walikimbia eneo la tukio,Polisi bado inawatafuta kufahamu kwa kina cha chanzo cha ajali hiyo kutokea.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

AMTOROKA MME WAKE NA KUKIMBILIA KUSIKOJULIKANA

AMTOROKA MME WAKE NA KUKIMBILIA KUSIKOJULIKANA                  ...